Hivi ndivyo Diamond alivyowa-sapraiz Mashabiki wake kwenye uzinduzi wa video ya Queen Darlin.

Ukubwa
wa jina la Diamond ndiyo hufanya mahali popote Tanzania anapotokea au
kuonekana kuwa na hali isiyo ya kawaida,Usiku wa kuamkia April 07 Club
Bilicanas kulikua na uzinduzi wa video ya Queen Darlin ambaye ni dada wa
Diamond Platnumz.
Wakati burudani zikiendelea mashabiki wakiwa hawajui kilichopo
backstage ndipo Diamond alipopanda kulitokea shangwe kubwa na kuna
shabiki mwingine alikuja kwa kasi kutaka kumkumbatia inawezekana ni
furaha iliyozidi kipimo kubwa zaidi ni shabiki ambaye alitoa machozi
kisa kikiwa ni kutaka kupiga tu picha na Diamond.
Hizi ni baadhi ya picha ya show hiyo zikimuonyesha na mastar kadhaa waliokuepo akiwemo Shettah.








0 comments:
Post a Comment