Dada mmoja aliyekuwa amepoteza wazazi wake baada ya ajali mbaya na akiwa
bila ya msaada huku ndugu wakiwa wamemkimbia, siku moja njaa ilimshika
na hakuwa na jinsi zaidi ya kupita nyumba kwa nyumba akiomba msaada wa
chakula.
Majirani wale hawakumpa chakula na kuamua kwenda
nyumba ya mwisho ambako mama wa nyumba ile alimfukuza binti yule huku
akisema hana chakula cha mchezo cha kumpa binti yule kwani chakula chake
ni cha tofauti na kisha akampiga na kopo tupu la maji na kumfukuza.
Binti kwa huzuni aliokota lile kopo tupu la maji na akaondoka kurudi
nyumbani kwake akipita uchochoro moja karibu na machimbo ya madini huku
akiufikiria mstari mmoja katika biblia wa Jeremia 29:11 usemao, "Maana
nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala
si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho"
Akiwa
anaendelea kuutafakari mstari ule mara lile kopo likaangukia kwenye
mfereji mmoja kwa kuwa dada alilihitaji lile kopo basi akalifuata pale
na kukuta limeangukia jirani na mfuko mdogo wa nailoni na ndani yake
akakuta kuna vipande viwili vya dhahabu vilivyofichwa.
Kwa yule
dada hii ilikuwa ni kama ndoto iliyokuja na kuwa ya kweli, akauza zile
dhahabu na kupata fedha nyingi ambazo kiasi akazitumia kwa kusaidia
watoto yatima na nyingine akafungua kampuni yake kubwa ya mavazi katika
mji ule kwa kuwa Mungu alimtendea miujiza.
Mungu wetu ni wa
baraka na miujiza, anaweza kukuinua kutoka sifuri na kukufanya uwe
shujaa mwenye kuheshimika na kuaminika hata pale inapoonekana kwako kuwa
ngumu kama utamtumaini na kuomba ulinzi wake daima.
Comment Amen kama unamtumaini na kuamini nguvu za Mungu katika kuyabadilisha maisha yako
Nakutakia usiku mwema na wiki hii kabla kuisha iwe ya miujiza ya mafanikio, amani na furaha kwako
Home »
»
0 comments:
Post a Comment