10 BEST MOVIES ZINAZOKIKI DUNIANI KWA SASA
Iwe kwa kuzishusha kwa torrent, kuzitafuta kwenye maduka au watembezaji wa filamu (japo ni rahisi kuzipata kwa sasa labda zile zenye kiwango cha chini) au kwa kwenda kuziangalia kwenye majumba ya sinema katika mji unaoishi, hizi ni filamu 10 zinazokiki kwa sasa duniani. Kwa wapenzi wa filamu hizi ni filamu za kuzitafuta na kuziangalia mwezi huu.
Captain America: The Winter Soldier
Ikiwa na wiki mbili tu tangu iingie sokoni, filamu hii iliyoongozwa
na Anthony Russo na Joe Russo imeshaingiza dola $159,006,000. Mastaa
waliocheza ni pamoja na Chris Evans, Scarlett Johansson, Samuel L.
Jackson na wengine.
Rio 2
Wapenzi wa katuni mpo? Hii ni filamu inayomake headlines kwa sasa.
Mastaa kibao wameweka sauti zao wakiwemo Anne Hathaway, Jesse Eisenberg,
will.i.am, Jemaine Clement, Tracy Morgan, George Lopez, Leslie Mann,
Rodrigo Santoro, Jamie Foxx, Andy Garcia, Rita Moreno, Bruno Mars na
Kristin Chenoweth.
Oculus
Kwa wapenzi wa filamu za kutisha hii ndio yenyewe ya kuitafuta.
Draft Day
Wapenzi wa filamu za vichekesho na michezo hii inawafaa. Mastaa
walioigiza ni pamoja na Kevin Costner, Jennifer Garner, Ellen Burstyn,
Denis Leary, Frank Langella, Chadwick Boseman na Sean Combs.

Divergent
Kwenye filamu hii utawaona Shailene Woodley, Theo James, Ashley Judd,
Jai Courtney, Ray Stevenson, Zoё Kravitz, Miles Teller, Tony Goldwyn,
Ansel Elgort, Maggie Q, Mekhi Phifer na Kate Winslet.

Noah
Russell Crowe, Jennifer Connelly, Ray Winstone na Emma Watson
wanaionesha dunia enzi za gharika na Nuhu ilivyokuwa. Kwa wapenzi wa
mikasa ya biblia hapa ndo penye!#

God’s Not Dead
Filamu hii ni ya comedy, drama na mambo ya familia.
Zingine ni pamoja na The Grand Budapest Hotel, Muppets Most Wanted na Mr. Peabody & Sherman.
0 comments:
Post a Comment