GUARDIOLA AZUNGUMZIA KUHAMIA KWAKE MAN UNITED, ASEMA...
KOCHA Pep Guardiola amekanusha tetesi za kuhamia Manchester United kutoka Bayern Munich anakopiga mzigo hivi sasa.
David
Moyes amefukuzwa leo United asubuhi na zikaibuka tetesi kwamba kocha
huyo Mspanyola anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba.
Lakini
Guardiola ameruka kimanga mapema, akizungumza na Waandishi wa Habari
katika mkutano maalum kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Hakuna kitu kama hicho: Pep Guardiola amesema anabaki Bayern Munich na kukanusha tetesi za kuhamia Manchester Untied
Amepigwa chini: David Moyes amefukuzwa baada ya karibu msimu mmoja wa kuwa kazini
Alipoulizwa
kama ana nia ya kuhamia United, Pep alisema: "Nipo hapa. Nipo Bayern na
ninataka kubaki kwa miaka miwili zaidi kumalizia kazi yangu. Tumeshinda
taji la Bundesliga, lakini nafikiri timu inaweza kufanya vizuri zaidi.
"Nafahamu
vizuri kutoka staili ya ligi ya Hispania na kubadilisha kwenye staili
ya Ujerumani haikuwa rahisi kwangu na ninahitaji muda zaidi ili kuhisi
hii ni timu yangu haswa.
"Nahisi
kweli Bayern ni timu yangu, lakini nafikiri tunaweza kucheza vizuri na
kuimarika. Kwa maana hiyo nafikiri nina kazi ya kufanya na ndiyo maana
ninataka kubaki zaidi hapa. Niko vizuri hapana watu wanaamini kazi
yangu,"amesema.
0 comments:
Post a Comment