TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI
Home » » Alichokisema NAPE NNAUYE kuhusu WEMA SEPETU kugombea UBUNGE

Alichokisema NAPE NNAUYE kuhusu WEMA SEPETU kugombea UBUNGE


BARAKA! Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.
Akistorisha na gazeti hili, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.

“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,” alisema Nape.

Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka 2010.

Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya Wema ni Ndumbagwe Misayo ëTheaí (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini)
Share this video :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | WILLE Template | GOOGLE
Copyright © 2013. Dj Wille Zedon - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger