Selecao walianza vizuri mchezo huo na kujitahidi kupeleka mashambulio makali katika lango la Paraguaay.
Mkongwe wa timu hiyo, Robinho alifanikiwa kuipatia Brazil bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Lakini goli hilo lilikuja kusawazishwa mnamo dakika ya 67 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa.
Brazil waliondoshwa katika matuta wakati Paraguay iliposhinda penati 4 huku Brazil ikipata penati 3 pekee.
Makali ya kinda wa Brazil aliyesajiliwa na Liverpool, Firmino yalishindwa kuonekana katika dakika zote alizocheza.
Kocha wa Brazil, Dunga ameisifu timu yake hiyo kwa kiwango kizuri lakini alilalamikia hali mbaya ya afya ya wachezaji wake ndiyo iliyopelekea kutolewa katika mashindano hayo.
Paraguay sasa itachuana na Argentina katika nusu fainali za mashindano hayo huku wenyeji Chile wakiivaa Peru hapo Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment