Akizungumuza na XXL ya CloudsFM, Diamond Platnumz amezungumzia mambo mbalimbali kuhusu Maisha yake katika Muziki, na hapa nimekuwekea Mambo manne muhimu aliyozungumuzia Diamond
1. Kuamini Uchawi
Diamond amedai Uchawi hupo lakini si vema kuuamini “Japokuwa vitabu vya dini vinasema ‘ndele’ zipo lakini haupaswi kuamini… Kuamini ni sawa na kumkiuka Mwenyezi MUNGU”
2. Kuhusu beef kati yake na Ali Kiba
Diamond amedai kwamba ajawahi kuwa na beef nae hata siku moja… na kuhusu Team za Mitandaoni Diamond amesema “Sioni kama kuna ubaya wowote, kila mtu ana maamuzi kumchagua mtu anayemtaka yeye kumshabikia, huwezi kumlazimisha mtu”
Wawachukue msanii fulani na msanii fulani wawashindanishe na wasanii wa nje, ukiwashindanisha wasanii wa Tanzania haiwezi kusaidia Industry yetu.
3.Kuhusu malipo ya collabo
Kumbe collabo za Dimond huwa alipi chochote “Sijawahi kufanya malipo kufanya nyimbo na mtu yoyote.. Mwanzoni ilikuwa tabu, sasahivi wanafahamu kwamba kufanya nyimbo na Diamond inakuwa rahisi nyimbo kufahamika East Africa… nimefanya collabo na karibuni wasanii wote wakubwa Africa.”
4. Kuhusu MTV MAMA
Hiki ndicho Diamond alichozungumzia kuhusu kuingia kwenye kinyang’anyilo cha MTV “Ni mwaliko wa MTV, wa kwanza nilipewa South Africa nikafanya vizuri, wakaona wanipe na sehemu nyingine”
“Wanaoona kuna umuhimu hizi Tuzo zije Tanzania waendelee kupiga kura, anayeona ni sawa kumpigia mwingine ni sawa… Uzalendo haununuliwi, huwezi kumlazimisha mtu”
“Muziki wetu umekuwa na nafasi nzuri sana Africa, ni kazi kubwa sana imefanywa… Kuna utaratibu unaandaliwa kuona kama tutaweza kuwabeba watu kama mashabiki na Watangazaji..
Tupige kura kwa siku hata mara moja sio mbaya, kama tulichukua ‘Channel O’ sasa hivi tutashindwaje”
0 comments:
Post a Comment