Rapa 50 Cent ambaye ni mmiliki wa lebel ya G Unit ameongeza orodha ya vipaji kwenye lebel yake baada ya kuingia mkataba na mwimbaji kutoka Nigeria Rotimi Akinosho.
Rotimi Akinosho ni kijana mwenye vipaji vya kuimba,kuandika muziki na kuigiza na kazi zake zitasimamiwa na G-Unit.
50 Cent mpaka sasa anaheshima ya kusimamia wasanii kama Lloyd Banks, Tony Yayo, Young Buck na Kidd Kidd. Rotimi na 50 cent wote wanaonekana kwenye tamthilia ya Power na Rotimi anaigiza kama Dre kwenye show hio.
0 comments:
Post a Comment