Msanii wa muziki wa Dance Hall kutoka Uganda Eddy Kenzo ameshinda tuzo ya Bet ya ‘Viewer’s Choice Best New International Artist’ mwaka 2015 kwenye tuzo zilizofanyika usiku wa jumapili ya 28 June 2015 kwenye ukumbi wa Microsoft Theatre huko Los Angeles Marekani.
Kenzo alikuwa akishindania tuzo hii na wasanii kutoka Afrika kusini Cassper Nyovest, Ghana ‘Mz Vee’ na watatu kutoka Uingereza ‘George The Poet, MIC Lowry na Novelist.
Kwanini ameshinda, Video yake ya 2014 ‘Sitya Loss‘ ilitazamwa na watu milioni 7 ndani ya mwaka mmoja tu ikiwa ndio video iliyotazamwa zaidi nchini Uganda na yatano Afrika Nzima.
0 comments:
Post a Comment