Mwimbaji kutoka Nijeria ‘Waje’ amesema alijiskia vibaya sana Psquare walivyopuuzia kumtaja kama msanii aliyeshiriki kwenye wimbo wao wa ‘Do Me’ uliofanya vizuri Afrika nzima mwaka 2008 kutoka kwenye album yao ya ‘Game Over‘.
Waje hakutajwa kama msanii aliyeshiriki kwenye wimbo na hata kwenye video hakuwekwa. Kwenye interview aliyofanyiwa hivi karibuni Waje amesema “Ukweli ni kwamba nilijiskia huzuni sana, nilikuwa underground na labda ningetokea kwenye video ningetoka mapema, ila nasmhukuru Mungu miaka kadha baadae niliweza kufanya na kutoka mwenyewe“.
Waje aliendelea kusema “P Square hawakunichukua walivyokwenda kufanya video Afrika kusini na hukujua kwanini hakwenda nao“.
0 comments:
Post a Comment