JE…!!! NIVEMA NA HAKI KUMPATIA MPENZI WAKO MAHABA WAKATI WOTE…!!!! SOMA HAPA
KATIKA mapenzi ya sasa, mahaba ‘chakula cha usiku’ yanapewa nafasi kubwa
sana katika kuleta furaha kwa wawili waliotokea kupendana kwa dhati.
Asikuambie mtu, kumnyima mpenzi wako penzi wakati anapolihitaji unamuumiza
kuliko maelezo na anaweza kufikia hatua ya kuhisi humpendi. Atafikiria hivyo
kwa kuwa umemnyima raha aliyotarajia kuipata kutoka kwako.
Hapa tunatakiwa kufahamu tu kwamba, furaha ya maisha ya binadamu yeyote
inakamilika kwa kuwa na mtu mwenye mapenzi ya dhati kwake na akapatiwa kila
alichotarajia yakiwemo ‘mahabati’. Katika siku za hivi karibuni kumeibuka
tatizo la baadhi ya wanawake kulia kunyimwa ‘mambo’ na waume zao.
“Mimi ni mwanamke bwana, nina hisia na kuna wakati najisikia kabisa hamu
ya kukutana na mume wangu faragha lakini sasa mume wangu akirejea nyumbani na
nikamwambia kuhusu hilo, anakuwa mkali, eti kachoka!
“Ingekuwa ni siku moja moja sawa lakini yeye kila siku akirudi anakula,
analala tena anageukia huko… inakuja kweli? Hivi na mimi nikisema nitafute
kidumu changu cha kuniliwaza pale ninapojisikia nitakuwa nakosea?” alilalamika
mama huyo.
Malalamiko haya yanaingia akilini licha ya kwamba mawazo aliyonayo Jastina
ambayo naamini wapo wengine walio katika mazingira kama hayo siyo sahihi. Mke
ana haki ya kupewa ‘chakula cha usiku’ na kama kuna sababu za msingi ni suala
la wawili kuzungumza na kuafikiana.
Kitendo cha mume kumbania penzi mkewe kwa maelezo kwamba amechoka kutokana
na kazi za kutwa nzima kinaweza kuchangia usaliti katika ndoa.
Najua katika maisha ya sasa watu hasa wanaume wanatumia muda mwingi sana
kusaka fedha kwa kufanya kazi na mwisho wake wakirudi nyumbani wanakuwa
wamechoka kiasi cha kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi. Lakini sasa ni sahihi
kwa wanandoa kukaa muda mrefu bila kupeana mambo? Jibu ni hapana!
Kama ni hivyo, nawashauri wanaume wanapofanya kazi wakumbuke kuna wake zao
wapendwa wanawasubiri nyumbani. Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake licha
ya kwamba kazi nayo ina umuhimu wake.
Pia kuna jambo ambalo wanaume na hata wanawake hawalijui vizuri, hili ni
lile linalohusu mazoezi. Unapofanya mazoezi unawezesha damu kuzunguka na kufika
sehemu zote za mwili kwa kiwango kinachotakiwa.
Kukaa ofisini kutwa nzima na kurudi nyumbani na kukaa kwenye kochi kisha
kuangalia TV siyo aina ya maisha inayoshauriwa tuishi. Mwili unapochangamka kwa
damu kufika kila mahali kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa ‘chakula cha
usiku’ na kukipokea huwa kubwa.
Lakini wanawake nao kuna wanaoishi kizamani sana. Hawa ni wale wanaosubiri
waume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata mwaka watakaa wakilalamika
kwamba hawapati ‘chakula cha usiku’.

0 comments:
Post a Comment