Mazingira yote yanaonesha wazi kuwa CHADEMA itashindwa vibaya Chalinze tarehe 6 mwezi huu kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge. Napata ujasiri na uhakika wa kulisema hili baada ya kulisoma onyo linalosambazwa na uongozi wa CHADEMA Taifa kwamba atakayeendelea kulalamikia ufinyu wa bajeti kwenye uchaguzi wa Chalinze ni MSALITI.
Sasa ni wazi kwamba Mbowe baada ya kulipwa amelazimisha mgombea kusimama katika jimbo hili ili kuzigawa kura za CUF hivyo kurahisisha ushindi wa CCM. Katika eneo hili CUF ilionesha kuwa na nguvu kama kweli tunachotaka kufanya ni kuiondoa CCM tulipaswa kuwaunga mkono CUF badala ya kutumika kugawanya kura za upinzani.
Ni aibu kwa mgombea wetu kuandaliwa mikutano ya watoto ilhali tunafahamu wazi kuwa watoto hao hawatapiga kura.
0 comments:
Post a Comment