Shilole katika picha ya pozi kwenye zulia jekundu
‘red carpet’.
Shamsa Ford akihojiwa kwenye zulia jekundu.
Steve Nyerere akikata keki.
Jana ilikuwa ni siku ya furaha kwa wasanii wa Kundi la Bongo Movie Unity
waliokuwa wakisherehekea kundi hilo kutimiza miaka mitatu tangu
lilipoanzishwa.
Sherehe za kumbukumbu hiyo zilifanyika kwenye Ukumbi wa Arcade,
Mikocheni jijini Dar ambapo wasanii walianza kwa
kupiga picha kwenye
zulia jekundu ‘red carpet’ na watu kibao waliohudhuria.
Kwa upande wa burudani ya muziki, wanamuziki Linex, Amini, Pendo wa
Maisha Plus, Shilole, Bendi ya Fm Academia na Bendi ya BM walitoa
burudani ya aina yake na kusababisha ukumbi wote kulipuka kwa shangwe.
0 comments:
Post a Comment