TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI
Home » »

 

 


Baadhi ya Wasanii  wa hapa nchini walizungumza na sammisago.com kwa njia ya simu akiwa  wakielezea juu ya kuguswa na msiba wa msanii nguli wa muziki wa Dansi Marehemu Muhidin Gurumo aliyefariki jana tarehe 13 April katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Afande Sele:
“Ni mamabo ya kumwachia Mungu  na Mzee alishakuwa Mtu Mzima na alikuwa anaumwa kwa muda mrefu, na hatuwezi kuongea kinafiki labda kama ni mshtuko sana kama ilivyotokea kwa kina Kanumba, Albert ambao ni vijana wadogo waliokufa bila kuugua yaani ghafla, Mzee Gurumo ni suala la kumuachia Mungu ni kusema tunamshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiyo ametoa na yeye ndiyo ametwaa, na alishafanya kazi nyingi sana ambazo zilimwekea heshima kubwa ndani na nje ya nchi, Kwa hiyo Mwenyezimungu kampenda zaidi”
ay
A.Y
Kwanza hata mimi mwenyewe nilipata taarifa na msiba kuupokea kwa mshtuko na kusema kweli ni mzee ambaye aliusukuma muziki tangu unavyoanza yaani, enzi za kina Baraka Mwishehe, na walifuata kina Mzee Gurumo na vile ambavyo mara ya mwisho nilimuona nilimchukulia kati ya wale watu ni kwamba taswira halisi ya Muziki wa Tanzania na sauti yake naamini itaishi miaka mingi sana na lamsingi ni kumwombea tu Mungu ampumzishe mahala pema peponi na tuzidi kumwombea na kuenzi muziki wake pamoja na familia yake na Band nzima ya Msondo”
mwasiti
Mwasiti:
“Kiukweli mimi kama Mwanamuziki  kama pia mwanamuziki Mchanga niseme hivyo,  Gurumo alikuwa Mwanamuziki Mkubwa sana, mimi niliweza kukutana naye kama mara mbili hivi pale THT kwa hiyo nilipata nafasi hiyo kupitia pale ni Mzee ambaye alikuwa anapenda watu na Mzee aliyekuwa anapenda Muziki wetu wa Bongo Fleva, pia ni Mzee ambaye ukikaa naye anakuambia muwekeze katika muziki kwa sababu aliona muziki wao na muziki wetu kuna tofauti kidogo sasa hivi wanapata pesa ya maana, pia nilikuwa nasikiliza nyimbo zake kwa muda mrefu sana tofauti na tunazozifanya sasa hivi kwa jinsi zilivyokuwa zinatufundisha. Kiukweli tumepoteza Hadhina kubwa sana katika muziki na  inabidi tuende kwenye msiba tukawafariji familia ya marehemu”
pina
Kala Pina:
“Kwa sisi ambao tupo kwenye tasnia nzima ya muziki ni pigo kubwa kwetu kutokana na Mzee wetu Gurumo ni moja kati ya wanamuziki wakongwe ambao wamefanya sanaa kwa miaka mingi na nyimbo zenye ujumbe wakuelimisha, kiukweli ameacha pengo ambalo sidhani kama kuna kitu atakayeweza kuja kuliziba katika tasnia nzima ya muziki, na ameweza kuweka histori kubwa sana ya kudumu kwa muda mrefu kwenye muziki, mimi naamini tupo kwenye msiba wasanii wote Tanzania nzima na tunaomboleza na tutakuwa wote pamoja kuhakikisha tunamzika Mzee wetu”
Msiba wa Marehemu Muhidin Gurumo upo numbani kwake maeneo ya Tabata Makubuli na mazishi hapo kesho taraehe 15 April katika makaburi ya Masaki huko Kisarawe Mkoa wa Pwani. Mungu ailaze roho ya Marehemu pema peponi Amen
Share this video :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | WILLE Template | GOOGLE
Copyright © 2013. Dj Wille Zedon - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger