HII NDIO BARUA NZITO KUTOKA GPL KWENDA KWA LULU, UNAWEZA ISOMA HAPA
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
KWAKO Elizabeth Michael ‘Lulu’. Leo nimeona
nikukumbuke kupitia barua! Natambua uwezo wako mkubwa katika kazi,
juhudi zako binafsi ndiyo zimekufikisha hapo ulipo, mataifa mbalimbali
sasa wanatambua kuwa kuna mtu anaitwa Lulu, yupo Bongo, muigizaji!.
Sitaki kukurudisha sana nyuma lakini najua unajua kuwa ni jinsi gani
kipindi cha nyuma ulikuwa ukipamba vyombo vya habari kwa skendo chafu.
Ulipoteza dira ya kimaisha, watu wengi waliokuwa wakikufuatilia kazi
zako walianza kukutupa.
Walikupotezea
kwa sababu ya matukio ya ulevi, mavazi ya nusu utupu na matukio mengi
ya ajabuajabu yaliyofanana na hayo. Sina nia mbaya kukumbusha lakini
waswahili wanasema binadamu anajifunza kutokana na makosa. Maishani
mwako umekutana na mazito yasiyofanana na umri wako.
Kwenye ulimwengu wa mahaba, ilikuwepo minong’ono mingi juu ya watu
wanaotajwa kushiriki mapenzi na wewe, walitajwa vigogo, mastaa na hata
wasio mastaa. Sitaki kusema ni kweli au la lakini lisemwalo kama halipo,
ujue laja.
Siri ilifichuka kupitia kifo cha yule unayedai alikuwa mwandani wako, marehemu Steven Kanumba.
Mazingira ya kifo chake, umri mdogo uliokuwa nao ilikuwa ni fundisho
kubwa maishani mwako. Ulipambana na msalaba wa gereza, ukapambana na
mlolongo wa kesi mahakamani hadi pale ulipofanikiwa kutoka kwa dhamana,
Januari mwaka jana.
Baada
ya kutoka mahabusu, kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa ulikuwa
kimya, ulionekana kubadilika kitabia. Yale uliyokuwa ukiyafanya awali,
uliyaweka pembeni na zaidi kusimamia mustakabali mzima wa maisha yako,
ulikuwa mwema sana aisee!.
Kinachonisikitisha ni kuanza kusikia tena matukio ya ajabu,
unaonekana kubadilika. Nimefuatilia tabia zako, naona umeanza
kubadilika, umesahau eeeh! Mavazi yako kwa miezi michache iliyopita,
nimegundua yanaanza kuchepuka! Mfano mzuri ni kigauni ulichokivaa
mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe yako ya kuzaliwa.
Hakikustiri maungo yako nyeti, kilionesha sehemu kubwa ya matiti yako.
Kama hiyo haitoshi, kupitia mitandao ya kijamii umeanza kushusha matusi
mazito bila sababu za msingi, mtu akikukosoa kidogo, unampa maneno
machafu ambayo hayaandikiki gazetini. Kama kioo cha jamii, unapaswa
kuvumilia mengi.
Nikiwa kwenye kazi zangu za kila siku, huwa nakuwa wa kwanza kupata
fununu za mabadiliko ya kila msanii na namna anavyoishi. Nikuonye tu,
kuwa makini na mwenendo wako kwani tayari jamii ilishaanza kujenga imani
na wewe. Uliaminika na ndiyo maana ukapata bahati ya kuchukuliwa katika
kampuni nzuri ikakusimamia kazi zako hadi sasa.
Kwa kuwa tayari nimeanza kupata malalamiko kutoka katika vyanzo
vyangu, nikusihi sana mdogo wangu, usirudi ulipotoka. Jenga heshima mpya
na jamii ikuamini kutokana na kazi zako na si skendo za ajabuajabu, kwa
leo ni hayo tu!
Wasalam.
Ni mimi Anko Erick Evarist.
0 comments:
Post a Comment