HILI NDO ZALI JINGINE LILILOMWANGUKIA LADY JAYDEE, NI KUHUSU KOMBE LA DUNIA. SOMA HAPA
Jaydee anayefahamika pia
kama Komandoo au Anaconda, amepata fursa ya kuandaa wimbo maalum wa
michuano hiyo ‘FIFA World Cup Anthem’ akishirikiana na wakali wawili
David Correy wa Brazil na rapa Octopizzo wa Kenya.
Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo 'akichana' kwa Kiswahili.
Wimbo
huo ulipigwa kwa mara ya kwanza jana jijini Dar es Salaam wakati
kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya
Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia
zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo
fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
Meneja Mkazi wa
Coca-Cola Tanzania, Yebeltal Getachew alisema hayo wakati wa hafla ya
uzinduzi ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam huku
akizitaja zawadi nyingine kuwa luninga, mipira na fulana.
“Mbali
na wateja 14 kupata nafasi ya kwenda Brazil, tutatoa luninga 1,000 za
kisasa zenye ukubwa wa inchi 32, mipira 8,000 yenye nembo ya FIFA World
Cup na T-shirt 30,000,” alisema Getachew.
Alisema kuwa kupitia Kombe la Dunia, kampuni hiyo itatoa sehemu ya mapato yake kwa jamii inayofanyia biashara.
Alisema
washindi watapatikana kwa kunywa vinywaji vya kampuni hiyo na kupata
vizibo viwili vinavyotengeneza neno ‘Brazil’ na kimoja cha ushindi
ambacho kitakuwa na picha ya kitu ambacho mteja wao atashinda.
Coca-Cola
ni mshirika wa FIFA wa muda mrefu tangu 1974. Kampuni hiyo ilianza
rasmi kudhamini Kombe la Dunia 1978 na uhusiano wao unatazamiwa
kuendelea hadi 2022.
0 comments:
Post a Comment