JOHARI ASEMA PENGO LA KANUMBA LAONEKANA!! NINI ZAID SOMA APA
Wikiiliyopita tulianza makala haya
yamhusuyo maisha ya msanii wa Filamu Bongo, Johari, sasa endelea
kufuatilia mahojiano yake mwandishi wetu Sifael Paul.
Sifael: Wewe ni miongoni mwa waigizaji wachache wakongwe, je, hadi sasa umecheza filamu ngapi?
Johari: Ni nyingi sana lakini nilizocheza kama main character (mhusika mkuu) ni zaidi ya filamu thelathini.
Sifael: Hapo katikati kulipita ukimya f’lani ukawa husikiki kabisa. Nini kilitokea?
Johari: Ni nyingi sana lakini nilizocheza kama main character (mhusika mkuu) ni zaidi ya filamu thelathini.
Sifael: Hapo katikati kulipita ukimya f’lani ukawa husikiki kabisa. Nini kilitokea?
Johari: Niliwapisha wasanii wachanga ili
wapate nafasi lakini walishindwa kwa sababu wameibuka watu ambao
hawakuwa serious na uigizaji badala yake walikuwa na lengo lingine
(kutafuta wanaume) so tasnia iliwashinda. Ndiyo maana nikaamua kurudi
kufanya kweli na tayari filamu zipo sokoni.
Sifael: Ukimya wako ulihusisha hadi
kutohudhuria matukio muhimu na hasa kwenye kumbukumbu ya miaka miwili ya
aliyekuwa mtu muhimu kwa tasnia, kama marehemu Kanumba. Kwa nini?
Johari: Nilikuwa nimesafiri kikazi kwenda mkoani Morogoro. Nilikuwa nashoot movie mpya. Siwezi kuitaja kwa sasa. Pia hapo katikati nilikuwa na project ya movie nilikuwa nafanya.
Johari: Nilikuwa nimesafiri kikazi kwenda mkoani Morogoro. Nilikuwa nashoot movie mpya. Siwezi kuitaja kwa sasa. Pia hapo katikati nilikuwa na project ya movie nilikuwa nafanya.
Kuhusu kumbukumbu ya Kanumba Aprili 7,
mwaka huu, nilirudi Dar ghafla kwa ajili ya hiyo ishu lakini bahati
mbaya nilichelewa kufika Dar Live (ukumbini).
Unajua inapofika siku kama hiyo
nakumbuka vitu vingi sana. Bado namkumbuka sana. Huwa nikimuwaza nalia
sana (akilengwalengwa na machozi). Mimi huwa simkumbuki Aprili 7 tu,
hapana, huwa namuenzi Aprili 7 hadi Aprili 11 (siku aliyozikwa kwenye
Makaburi ya Kinondoni, Dar).
Sifael: Kutokuwepo kwa Kanumba kuna madhara yoyote kwa tasnia ya filamu?
Johari: Katika sanaa kila mtu ana nafasi yake kwa namna alivyojitengenezea mashabiki wake. Watu wanaweza kummisi Kanumba zaidi lakini sisi RJ Productions (kampuni yake na Ray) tunammisi zaidi.
Johari: Katika sanaa kila mtu ana nafasi yake kwa namna alivyojitengenezea mashabiki wake. Watu wanaweza kummisi Kanumba zaidi lakini sisi RJ Productions (kampuni yake na Ray) tunammisi zaidi.
Unataka kujua kwa nini? Tumekosa
ushindani. Kama utakumbuka kulikuwa na ushindani mkubwa sana kati ya RJ
na Kanumba The Great. Sasa hivi hakuna kampuni ya kushindana na RJ.
Angali kampuni nyingi za filamu. Sioni ambayo inaleta changamoto.
Sifael: Ni changamoto gani unakutana nazo kwenye tasnia ya filamu?
Johari: Changamoto kubwa ni kukosa mshindani halafu ndiyo linakuja suala la serikali kutambua Bongo Movies kuwa inatoa ajira kwa watu wengi hivyo kuwe na sapoti ya kutosha.
Johari: Changamoto kubwa ni kukosa mshindani halafu ndiyo linakuja suala la serikali kutambua Bongo Movies kuwa inatoa ajira kwa watu wengi hivyo kuwe na sapoti ya kutosha.
Sifael: Kuna watu wanaamini kuwa kifo cha Kanumba kimeua tasnia ya filamu. Je, ni kweli?
Johari: Kwa mtazamo wangu hiyo ni kauli ya watu wenye akili finyu.
Johari: Kwa mtazamo wangu hiyo ni kauli ya watu wenye akili finyu.
0 comments:
Post a Comment