Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, amesema kuwa amesema wachezaji wake, Juma
Kaseja na Emmanuel wana matatizo binafsi ndiyo maana akaamua kutowatumia kwenye
mechi dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, jana.
Kocha huyo raia wa Uholanzi amesema kuwa Kaseja na Okwi hawakuwemo
kwenye kikosi chake kwa sababu hakuwa nao hata mazoezini, hivyo hawezi kumtumia
mchezaji ambaye hajafanya naye mazoezi na kusisitiza kuwa wawili hao wana
matatizo yao binafsi kama inavyoripotiwa.
“Sikuwa nao kwenye mazoezi, ndiyo maana sijawatumia, wana matatizo yao
binafsi kama ambavyo inaandikwa kwenye magazeti, siwezi kulizungumzia zaidi
hilo, lakini ifahamike hivyo,” alisema kocha huyo bila kuwa tayari kufafanua
matatizo yapi.
Okwi amekuwa nje ya kikosi hicho kwa siku kadhaa sasa ikiripotiwa kuwa
ana madai yake ya fedha ambayo hajakamilishiwa mpaka sasa wakati wa usajili,
huku taarifa za ziada zikisema kiasi ambacho anadai ni shilingi milioni 60,
wakati Kaseja haijajulikana matatizo yake.
0 comments:
Post a Comment