Profesa Jay kuachia album (double CD) ya ‘The Best of Profesa Jay’
Profesa amesema album hiyo itakuwa na takriban nyimbo 30.
“Nina mpango wa kufanya double CD ya The Best of Profesa Jay, ambayo itakuwa na takriban nyimbo 30, yaani fifteen, fifteen. Nyimbo za zamani zitachanganyika na za sasa lakini zitachanganyika na ambazo hazikutoka (unreleased) pia,” alisema.
Hata hivyo Profesa ambaye kwa sasa ana wimbo mpya uitwao ‘Kipi Sijaskia’ aliomshirikisha Diamond, amsema bado yupo kwenye wakati mgumu kuchagua nyimbo 30 bora zaidi katika zote alizowahi kurekodi kwakuwa nyingi ni nzuri.
Profesa ameongeza kuwa pamoja na album hiyo ya mkusanyiko wa nyimbo zake, atazitoa tena album zake zamani kuziingiza sokoni ambazo ni pamoja na Machozi Jasho na Damu, Mapinduzi Halisi, J.O.S.EP.H na Alua Continua na kwamba ataziweka kiwango kizuri zaidi.
“Tunafanya mpango wa kuziremaster zile sababu nyingi zilikuwa na quality mbovu wakati ule bado tulikuwa hatuna uwezo wa vifaa vya ziada. Tunataka tuzileke Canada zile album kuziremaster, tunafanya mastering tena ili ziwe ziweze kuwa na quality ambayo inaweza kwenda kwenye soko la ushindani ambalo lipo,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment