Makala] Maana/Tafsiri ya Tattoo za Diamond, Uwoya, Wema na Mastaa Wengine wa Bongo
Kama tungekua nchi za wenzetu tukaanza kuandika kuhusu tattoo na
wasanii basi tusingemaliza leo, maana karibia kila msanii ana tattoo na
sio moja tu bali zaidi ya moja. Lil Wayne ana zaidi ya tattoo 300 , Rihanna ana tattoo 19 ,Miley Cyrus ana tattoo 19 na Bruno Mars akiwa
na Tattoo 5 . Tattoo imekua ji mfumo ambao wasanii wengi sana duniani
wamekua wakiutumia kuandika miili yao kwa maana fulani au basi tu
urembo, kuna wasanii kama Birdman “Baby” Cash Money Records CEO ambae
yeye na mwanae wa kufikia Lil Wayne wana tattoo mpaka usoni kuchora
matone ya MACHOZI kwa kila mtu ambae ni muhimu kwao aliewatoka
(kufariki) na hii ni kumaanisha kuwa bado wanawalilia. Kwa mujibu wa
wataalam wanasema Tattoo ni “Addiction” ukianza na moja tu, utajisikia
kuchora nyingine na nyingine na utakuta zinaongezeka mwilini na hii ni
sababu ya kupenda zinavyoonekana au starehe ya maumivu wakati inachorwa.
Lakini vipi kwa upande wa bongo? Tattoo na usanii au umaarufu
vimeanza kuendana hapa bongo baada ya sanaa kuanza kutambulika na sana
sana ya wasanii wa BongoFlava, zamani tattoo walikua wanachora Mabaharia
wanaofanya kazi kwenye Meli kubwa na wao walikua wanaiga desturi za hao
wanaowaajili kwenye Meli hizo, kwa hiyo kwa hapa nchini kuanzia miaka
ya 80 tattoo maarufu sana zilikua “NANGA” ya Meli, Nyoka ajulikanae kama
“COBRA”, “bleeding Heart”, “Eagle” na hizi zote zilikua ni tattoo
zilizoletwa na Mabahari watanzania wafanyao kazi kwenye Meli za Kigiriki
na nyinginezo za Bara la Ulaya.
Hii ni list ya wasanii wa bongo wenye tattoos.
Diamond Platnumz
Diamond PLATNUMZ ana tattoo kubwa kwenye mkono wake wa kulia maeneo
ya begani na nyingine kwenye mkono wake wa kushoto yenye maandishi ya
kichina ambayo maana yake ni “I Love U Mama”, sijui ni kwanini ameamua
kuandika kwa Lugha ya kichina ila kwa maoni yangu ingependeza zaidi kama
angetia lugha anayoitumia yeye ya nchini kwake kama “Nakupenda Mama”
ingependeza zaidi.
Wema Sepetu
Wema SEPETU ni moja kati ya wasanii wa bongo wenye tattoo nyingi ,
ana tattoo kwenye shingo yake , pia ana tattoo yenye maandishi ya
kichina mgongoni yenye maana ya “potential” kwa lugha ya kiingireza. pia
ana tatoo mkononi na kwenye bega. na zaidi ya hapo hana tattoo nyingine
sehemu ambayo inaonekana wazi labda kwingine ambako hatuwezi kuona au
kuonyesha kwenye PUBLIC maana katika mwili wa binadamu kuna sehemu
“Potential” nyingi sana ambazo tattoo inaweza kukaa vizuriiii kabisa na
kuonyesha MVUTO wa hali ya juu.
Ney wa Mitego
NEY Wa MITEGO ni mmoja kati ya wasanii wabishi wanaofanya muziki
mgumu maarufu kama Hip Hop, ambaye amejaribu kubeba dhana hiyo kama
msanii anayetafsirika kimuonekano, Ney wa mitego ameanza kuchora tattoo
tokea mwaka 2002 alipokua kidato cha pili katika shule ya sekondari ya
mbezi beach. Katika mkono wake wa kulia kuna tattoo yenye nanga ya “HIP
HOP” ikiwa na maana kuwa yeye ni mtu mwenye imani na ndoto za kufanikiwa
kupitia muziki huo wa ‘Hip Hop’, ‘tattoo’ iliyopo katika mkono wa
kushoto ni nyoka mwenye mabawa (Dragon) , Dragon ni kiumbe ambacho ni
adimu kuonekana duniani na kinachoabudiwa sana barani Asia sana sana
China na Korea.
.
.
Elizabeth Michael “Lulu”
ELIzABETH “Lulu” MICHAEL naye hayupo nyuma katika kuchora tattoo.
Lulu ni msanii ambaye anakua ndani ya sanaa na ana fursa kubwa sana
kujifunza mambo mengi taratibu kutokana na Umri wake na ukuaji wake
ndani ya sanaa, Lulu ni msichana ambae tunamtegemea sana kufikisha
tasnia hii ya Filamu mbali sababu kwake yeye ni kama yupo Darasani
maishani kusoma maisha na tasnia pia. Ni matarajio makubwa sana aweze
kujifunza vyema na kuweza kuifikisha Tanzania katika nyanja za juu za
Filamu kama wasanii Lupita Nyongo wa Nchini Kenya. kwa upande wa Lulu ni
kidogo na ni tofauti na wengine kwani yeye ameamua kuweka ujumbe wa
maneno chini kidogo ya shingo lake karibia na bega unaosema “Only God
can Judge Me” hii inamaanisha ni “Mungu Pekee ndio atakae nihukumu”
.
.
Jux
Jux VUITTON ana tattoo mbili, Ya kwanza ipo kifuani na watu wengi
wamekuwa wanasema tattoo hii inafanana na ile ya “Trey Songz” msanii wa
mindoko ya RNB nchini Marekani ambae nae aliwahi kushukiwa kuwa style
yake ya uiambaji anamuiga msanii mkongwe wa miondoko hiyo R KELLY.
Tattoo hiyo ya JUX lakini ukweli ni kuwa sehemu ya mwili aliyoichora ni
kama ya msanii Trey Songz lakini fonts na ujumbe ni tofauti kwani
tattoo ya msanii huyo ameandika ameandika kwa ajili ya mama yake , mdogo
wake wa kiume na bibi yake huku kwa upande wa JUX ukiwa na ujumbe mzito
pia lakini hatujajua bado unamhusu nani na part ya tattoo hiyo inasema
“ALWAYS MISSING YOU” na “HOPE TO SEE YOU”. Jux ana tattoo nyingine
mkononi maeneo ya bega ikiwa na “Virgo Angel” kwa kibongo tunaweza
ambayo kwa lugha ya kiswahili inajulikana kama mashuke .
Irene Uwoya
Irene UWOYA nae ni kati ya wasanii wakubwa wakwanza kabisa kunyesha
tatoo zake katika mwili wake, UWOYA ana tattoo juu kidogo ya matiti yake
yenye alama ya nyayo za paka au chui ambapo tattoo hii ilikua maarufu
sana miaka ya 90 ambayo tattoo hiyo ilivhorwa na mwanadada msanii wa
miodoko ya Hip Hop nchini Marekani “EVE”. Tattoo hii ilikua maarufu sana
na wanadada wengi sana duniani waliweza kuchora tattoo hii sababu ndio
ilikua HOT kipindi hicho kutokana na msanii huyo. Pia UWOYA ana tattoo
mgongoni iliyoandikwa krrish ikiwa na alama za nyayo ya mtoto mdogo ambayo ni maalumu kwa ajili ya mtoto wake Krrish Ndikumana.
Kuna tattoo nyingine zinaonekana kiunoni na miguuni pia ila sehemu
nyingine zinahitaji kazi kubwa sana kuweza kuziona vizuri na kuweza
kupata maelezo kamili au hata picha zake ili kuweza kushare na
0 comments:
Post a Comment