BI MWENDA AMZIMIKA PROF. JAY
NAKUKUBALI! Mkongwe kwenye soko la filamu za Kibongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ amefunguka kuwa anamzimika kinomanoma mkali wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule ‘Prof Jay’ kutokana na tungo zake mahiri.
Bi Mwenda aliitoa kauli hiyo Jumatano iliyopita katika hafla ya Uzinduzi wa Global TV Online iliyofanyika katika Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge ambapo wasanii mbalimbali wa filamu na muziki akiwemo Prof Jay, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, Issa Musa ‘Cloud 112’ na wengine kibao walihudhuria.
“Oooh! Jamani ndiyo mara ya kwanza namuona Prof. Jay kwa macho yangu, kiukweli nakubali sana kazi zake, ni mtunzi mzuri, mwimbaji na hata nyimbo zake huwa zina ujumbe sana,’’ alisema Bi Mwenda.
0 comments:
Post a Comment