MUCHACHO WA SIMBA AFARIKI DUNIA, KUZIKWA LEO DAR
Mwanzilishi wa kundi maarufu la ushangiliaji la klabu ya Simba, Abrahman Muchacho amefariki duniani jijini Dar es Salaam.
Muchacho ambaye pia ni shabiki namba
moja wa timu ya soka ya Liverpool ya England amefariki duniani leo na mazishi
yake yamefanyika mchana huu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia,
Muchacho alitarajiwa kuzikwa mchana wao leo kwenye makaburi ya Kisutu jijini
Dar es Salaam.
Kengete Blog inatoa pole kwa wanafamilia ya Muchacho pamoja na Wanasimba wote, lakini inasisitiza kuwa ni wakati wa kufuata mfano wake wa uzalendo kwa timu yake, ndiyo maana alitaka ifanikiwa na akaamua kuanzisha kikundi cha ushangiliaji. Nani mwingine anabuni nini ili kumuenzi?
0 comments:
Post a Comment