ROONEY FITI KABISA, AWAPASHIA KIKAMILIFU BAYERN MUNICH LEO
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amerejesha
matumaini ya Manchester United kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya baada ya kuanza mazoezi kwa ajili Robo Fainali ya pili dhidi ya
mabingwa watetezi, Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena kesho.
Rooney alikosa mechi ya Ligi Kuu England
United ikiifunga mabao 4-0 Newcastle mwishoni mwa wiki kutokana na
maumivu ya mguu, lakini sasa kuna uwezekano kesho akacheza
Ryan Giggs pia alifanya mazoezi baada ya
kukosa mechi dhidi ya Newcastle, lakini Marouane Fellaini, ambaye
alitolewa nje Uwanja wa St James Park baada ya kuumia na Rafael
hawakushiriki mazoezi leo.
Baada ya sare ya 1-1 nyumbani, United sasa wanatakiwa kushinda ugenini dhidi ya Bayern ili kutinga Nusu Fainali.
Mazoezi makali: Rooney akifanya mazoezi kuelekea mchezo wa marudiano na Bayern Munich
Rooney alishiriki mazoezi kikamilifu
Rooney ameonekana kusahau kabisa kuhusu maumivu
Rooney ameonekana yuko fiti kwa ajili ya mchezo huo
Kocha wa Manchester United, David Moyes ameonekana kufurahia kurejea kwa Rooney
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni
Links to this post