Ligi kuu Tanzania bara imeendelea jioni ya leo katika viwanja viwili
tofauti ambapo kwenye uwanja wa Taifa, Yanga ilikua mwenyeji wa Kagera
Sugar huku kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga wenyeji Mgambo JKT walikuwa
wakiikaribisha Simba.
Kwenye uwanja wa Taifa Yanga wamerejea katika usukani wa ligi hiyo na kuishusha Azam kileleni kwa kufikisha pointi 34 nyuma ya Azam wenye pointi 33 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa.
Wakicheza kwa kujiamini Yanga wanaanza kwa kufanya mashambulizi makali ambapo dk ya 6 Simon Msuva anaangushwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi anasema ipigwe penalti ambapo dk8 anaifungia Yanga goli la kwanza. Dk 14, Tambwe anaifungia Yanga bao safi la pili baada ya Ngassa kuwazidi mbio mabeki wa Kagera na kupiga krosi safi. Dk 39, Salum Kanoni anaifunga kwa uzuri kabisa Kagera kwa njia ya penalt akimchambua Barthez baada ya Atuplele Green kuangushwa eneo la hatari.
Kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga, Simba wanaonja machungu baada ya kuruhusu kuchapwa mabao 2-0 dhidi ya Maafande wa Mgambo JKT.
Simba ambao walianza kwa kuwakamia zaidi wapinzani wao bahati haikuwa upande wao ambapo dk ya 45 Ally Nassor anaifungia Mgambo bao la kwanza baada ya kupiga shuti kali huku kipa wa Simband Ivo Mapunda akiwa amezubaa Dk 63, Ivo Mapunda analambwa kadi nyekundu na Mgambo wanapata penalti baada ya yeye kumuangusha mshambuliaji wa Mgambo ambapo dk 67 Fullyzully Maganga anafunga penalti na kuiandikia Mgambo bao la pili.

0 comments:
Post a Comment