
Mashabiki wengi wa ndondi duniani bado wanahamu ya kutaka kujua je ni
mwanamasumbwi gani atapambana na mkali wa mchezo huo kutoka marekani
Floyd Mayweather ambapo hilo ndilo litakua pambano la mwisho kwa Floyd
mayweather kwani baada ya hapo anastaafu rasmi kucheza mchezo huo.
Floyd Maywether pambano lililopita alimtwanga Mphilipino Manny Pacquayo
ambapo baada ya hapo tetesi zilizagaa kwamba wawili hao wanaweza
kurudiana kwenye mpambano wa mwisho wa Mayweather.
Lakini uvumi huo ulipotea ghafla mara baada ya kujitokeza kwa bondia
Amir Khan ambaye alisema yupo tayari kupambana na Maywether kwenye
pambano lake la mwisho.
Ukimya ulizidi kwani hakuna lolote lililoendelea na kuonyesha kwamba Amiri Khan atapigana na Maywether.
Lakini habari zilizovuja hapo jana ni kwamba Floyd Maywether
ameamuakumchagua bondia De La Hoya ili apigane nae kwenye pambano lake
la mwisho hapo mwezi septemba.

Endapo mambo yakiwa sawa, basi wawili hawa watakua wanarudiana kwani
walishawahi kupigana mwaka 2007 na Floyd maywether aliweza kuibuka na
ushindi wa point.
0 comments:
Post a Comment