Jana kwenye Hekaheka ilikuwa ishu ya mwanamke mmoja ambae alipata ujauzito wa mwanaume mwingine wakati mume wake ambae ni mwanajeshi akiwa nje ya nchi kikazi.
Ishu ilifika Hospitali ya Mwananyamala ambao waliwaambia wampeleke mtoto huyo Polisi ili apelekwe Ustawi wa Jamii.. Mama wa mtoto huyo hakutaka mtoto wake apelekwe Ustawi wa Jamii.
Walivyofika Polisi waliongea ukweli, Polisi wakataka kuwakamata kwa kesi ya kuidanganya Serikali, lakini baadae wakaachiwa na mtoto.
Mama mzazi mwenye mtoto huyo amesimulia jinsi ilivyokuwa… amesema hawezi kurudi kwa mumewe kwa kuwa ni mkali anaweza kumpiga.
Yeye na mume wake huyo mwanajeshi wana watoto watatu, amesema hawezi kurudi watoto watalelewa na baba yao.
Hekaheka iko hapa, utasikia wahusika wote wakisimulia ishu ilivyokuwa.
0 comments:
Post a Comment