Messi achangiwa fedha na Yanga MASHABIKI wa Yanga, jana Jumanne walimpatia fedha kiungo wa Simba, Ramadhan Singano ‘Messi’ wakati alipoingia kwenye eneo la Karume ambapo timu yao ilikuwa ikifanya mazoezi yao ya kwanza.
Mambo yalikuwa hivi! Yanga jana ilikuwa ndiyo siku yao ya kwanza kuanza mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam majira ya asubuhi na Singano alikuwa anatakiwa kuingia kwenye ofisi za Karume kwa ajili ya kujadili mgogoro wake wa kimkataba na viongozi wa Simba.
Messi na Simba wapo kwenye mgogoro wa kimkataba ambapo jana Jumanne TFF iliwaita wawakilishi wa pande zote mbili kuzungumza na kumaliza mgogoro waliokuwa nao.
Baada ya Messi kuingia, mashabiki wa Yanga walimuona akiwa kwenye gari lake aina ya Mazda na kuanza kumshangilia kabla hawajakubaliana kuchangishana fedha na kumpa huku wakiwa wamelizingira gari lake hali iliyomfanya ashindwe kwenda nyuma au mbele.

0 comments:
Post a Comment