Heka heka za wananchi kutaka kuzuia msafara wa Mh.Lowasa zilianza mapema asubuhi wakati anawasili kwenye uwanja wa ndege wa musoma ambapo vijana walizuia msafara wake kutoka kwenye uwanja huo wakitaka wapewe nafasi ya kuonana naye.
Baada ya waratibu wa msafara huo kufanya kazi ya ziada ya kufanikiwa kutatua changamoto hiyo Mh.Lowasa aliekea katika wilaya ya Bunda na licha ya kusimamishwa na wananchi njiani hali ilikuwa ngumu zaidi katika ofisi ya CCM wilaya ya hiyo kutokana na watu kujitokeza kwa wingi.
Hata hivyo pamoja na maelfu ya wananchi hao wanaounga mkono safari ya matumaiani kuwa na shauku ya kumueleza Mh.Lowasa shida zao alishindwa kuwasikiliza kutokana na kubanwa na kanuni na aliwaomba kuwa watulivu na kuendelea kuiombea kheri safari ya matumaini.
Mh.Lowasa akiwa katika mkoa wa Mara amepata idadi kubwa ya wadhaamini pia amefika nyumbani kwa hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere na kupewa baraka, kisha kuweka shada la maua kwenye kaburi na pia ametembelea wilaya ya Tarime na Musoma.
Mh.Lowassa ambaye ameshatembelea mikoa ya Mwanza Geita,Zanzibar na Pemba anaendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mkoa wa Simiyu.

0 comments:
Post a Comment