TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI
Home » » Maneno ya Wema Sepetu Baada ya Kutuhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mume wa Linah

Maneno ya Wema Sepetu Baada ya Kutuhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mume wa Linah

Maneno ya Wema Sepetu Baada ya Kutuhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mume wa Linah
 
Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema Sepetu kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu!

Wiki iliyopita zilisambaa picha mtandaoni zikimuonyesha Wema Sepetu akiwa amepozi kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.

Katika maelezo yake kuhusiana na kusambaa kwa picha hizo, Wema amesema kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu, hivyo Linah asiwe na shaka naye hata kidogo.

“Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga na marafiki wengine kama akina Martin Kadinda, Petit Man na wengineo. Sina uhusiano naye wa kimapenzi, naomba aamini kuwa ni rafiki tu wa kawaida,” alisema Wema na kuibua maswali juu ya aina ya uswahiba wa kawaida wa kupiga picha kitandani na mpenzi wa mtu!

Share this video :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | WILLE Template | GOOGLE
Copyright © 2013. Dj Wille Zedon - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger