Manchester United yafikia makubaliano na Real Madrid juu ya dili hili…
De Gea atakamilisha uhamisho wake kwenda Hispania baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa Jumapili hii na atakapotua Real Madrid, Casillas ataondoka klabuni hapo baada ya kudumu kwa miaka 16.
Casillas (kulia) anaondoka kumpisha De Gea (kushoto)
Klabu za Manchester United na Real Madrid zimekubaliana kufanya dili la golikipa wa Old Trafford, David de Gea.
Kwa maana hiyo Iker Casillas anakaribia kuondoka Real Madrid kumpisha De Gea kuwa kipa namba moja mara tu ataposaini mkataba wa kutumika Bernabeu wiki ijayo.
De Gea atakamilisha uhamisho wake kwenda Hispania baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa Jumapili hii na atakapotua Real Madrid, Casillas ataondoka klabuni hapo baada ya kudumu kwa miaka 16.
Casillas ambaye ameweka historia kubwa Real Madrid amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa na anataka kulipwa fidia yote endapo anatimka.
0 comments:
Post a Comment