Mwanadada anayekuja kwa kasi katika muziki wa bongo, Dayna Nyange,
ameiomba jamii isimfikirie vibaya kuhusu wimbo wake wa Nitulize.
Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya jamii kuhoji picha ya kava ya wimbo huo akiwa na Ney wa Mitego.
Dayna, alisema yeye ni mcha Mungu na amelelewa katika maadili mema.
Kava la wimbo Nitulize wa Dayna na Ney
Dayna ameingia matatani baada ya kava hiyo kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake.
Dayna alisema kazi ya muziki imekuwa ikimweka katika wakati mgumu kutokana na jamii kutambua kuwa ni mcha Mungu.
“Kazi ya muziki inafanya nionekane mtu wa ajabu wakati nimelelewa kwa
malezi mazuri naomba jamii itambue hilo na isiwe na shaka na mimi,”
alisema Dayna.
0 comments:
Post a Comment