Kila msanii a mipango yake…Mipango ya Nahreel ni kufungua chuo cha muziki ambacho kitawasaidia vijana kufanya muziki kitaalam zaidi. Jina la chuo hicho ni The Industry Music School (IMS)
Akizungumza katika kipindi cha XXL …Nahreel amesema “Classes zitaamza karibuni tu..tutakuwa tunauwezo wa kuchukua wanafunzi wengi tu na kuwafundisha kwahiyo haya madarasa yataanza soon tu na tutatoa taarifa…..Kwanza hatutakubali kuanza kuchukua mwanafunzi yoyote tu, tutaanza kuzingatia kwanza mwanafunzi lazima kidogo awe na uelewa wa muziki kidogo hata kama hajawahi kufanya muziki basi awe anaupenda muziki, kwahiyo tutafanya audition ili tuepuke usumbufu wa kufundisha tu watu fulani ambao hawataweza kufanya vitu ambavyo tunafundisha…Shule itakuwa ni miezi mitatu kwa kozi moja, na nimpango wa kuwa na wanafunzi 30 mpaka 40 kwa hiyo semester.”
0 comments:
Post a Comment