KUMBE WIMBO ULIOTAMBULISHWA MITANDAONI NA KUSAMBAA KWA KASI SANA KUWA NI WA ALI KIBA UMELETA KIZAA ZAA, WATU WAME COPY MPKA SAUTI...LOL!! ALI KIBA KAFUNGUKA NA KUKANA VIKALI..SOMA HAPA
Sina shaka kama wewe ni shabiki wa Alikiba hukujiuliza mara mbili kuupakua wimbo wa ‘Rosa’ ambao umesambaa wiki hii katika mitandao kama comeback ya star huyo aliyekaa kimya kwa muda mrefu. Lakini cha kushangaza ni kuwa Alikiba mwenyewe hautambui wimbo huo sababu hauko kwenye orodha ya nyimbo alizowahi kurekodi na wala hafahamu mtu aliyeuimba.Alikiba amesema amepigiwa simu na vituo vya redio vikimuuliza kuhusu wimbo wake mpya walioupata uitwao ‘Rosa’ lakini hana taarifa nao.
“Nyimbo zipo lakini sija release nyimbo…sijatoa nyimbo so far na sijui nani ameimba na sijawahi hata kuisikia” Alisema Alikiba alipozungumza na
“Sijawahi kuisikia na sitaki kutoa comment yoyote kwasababu navyojijua mimi first of all najikubali sana, la pili watu wananiambia niko unique afu surprise watu wananiambia nimetoa nyimbo sijui tumesikia nyimbo inaitwa Rosa yaani hiyo sijaelewa bado.” Alisema hit maker wa Cinderella.
Aliongeza kuwa kuna uwezekano kuwa kuna watu wamefanya makusudi kufake wimbo huo uonekane ni wake kutokana na ukimya wake, au wamefanya sayansi sauti isikike kama yake, au huyo aliyeimba ni role model wake ndio sababu kaamua kufanya hivyo.
“Wameona nimekaa kimya sana wakaona ngoja watoe nyimbo na wakatumia jina la Alikiba, it doesn’t make sense kama unatoa nyimbo unategemea kutoka kwa jina la mtu flani, I think ni trick moja ambayo imefanywa sielewi na nani lakini I don’t know if in a good way or bad way.”
Pia Ali K alizungumzia ujio wake mpya,
“Ujio wangu uko very soon, sasa hivi wakae tayari fans wangu na kilichonifanya nikae kimya kingi watajua ni kitu gani na watani understand kabisa maana ya kukaa kimya.”
Msikilize hapa
Huu ndio ‘Rosa’ wimbo ambao Alikiba amedai haujui
0 comments:
Post a Comment