Jokate Mwegelo adai bado yupo single....Kazi kwenu akina kaka
Jokate Mwegelo yupo single ... Staa huyo mwenye vipaji lukuki alisema hayo Jumatatu hii kwenye kipindi kipya cha TV1, ‘The One Show’ anachokiendesha kwa kushirikiana na Ezden Jumanne aka The Rocker.
Katika kipindi hicho cha kwanza kuoneshwa, watangazaji hao walianza
kwa kuhojiana wao kwa wao kwanza na moja ya maswali aliyoulizwa Jokate
ni kama yupo kwenye uhusiano wowote wa mapenzi. Jokate ambaye pamoja na
kuwa muigizaji wa filamu pia ni muimbaji wa muziki na mjasiriamali,
alisema kuwa kwa sasa yupo single lakini haimaanishi kuwa wanaume
hawamsumbui kumtaka kimapenzi.
Jokate amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa
basketball wa timu ya Oklahoma City Thunder, Mtanzania Hasheem Thabeet
pamoja na uhusiano uliodumu kwa kipindi kifupi na staa wa muziki,
Diamond Platnumz.
0 comments:
Post a Comment