kwa sababu alimbiwa na Mungu asioge
Mchungaji adai hajaoga tangu mwaka 2001 kwa sababu alimbiwa na Mungu asioge
Nadhani ulishawahi kusikia ama kushuhudia watu wa eneo Fulani ama jamii fulani wakimlazimisha kichaa kuoga kwa nguvu kwa kuwa amezidi kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa waumini wa dhehebu analolisimamia mchungaji Wale Olanguji wa Nigeria.
Mchungaji Wale wa kanisa la Divine Seed of God wa Ibadan, Oyo,
Nigeria ameliambia jarida la People City la Nigeria kuwa hajawahi kuoga
tangu mwaka 2001 wakati ambapo anadai alipokea amri ya Mungu ikimtaka
afanye hivyo na kwamba ajitenge na mkewe na kuacha kutumia baadhi ya
vinywaji.
Cha ajabu, licha ya kukaa miaka 13 bila kuoga mchungaji huyo hatoi
harufu na ni vigumu kumshitukia hadi akuoneshe mwenyewe vielelezo!
Hivi ndivyo mchungaji huyo alivyoliambia jarida hilo wakati
lilipomkumbusha kuwa mwaka 2001 alitoa maelezo kuwa Mungu amemwambia
asioge:
"Ndiyo, ni miaka 13 hadi sasa kwa ufupi. Mwaka 2000 mwanzoni Mungu
aliniambia niache kuoga, nijitenge na mke wangu na kwamba natakiwa
kuacha kutumia vinywaji vyote laini pamoja na wines. Na tangu wakati
huo…kwa kweli, nimekuwa nikifuata yote hayo.
"Mtu yeyote ambaye Mungu anataka kumtumia kwa sababu hapa duniani,
kuna gharama imeambatanishwa kwenye huo wito. Kwa hiyo ninaamini kwamba
hiyo ni gharama ninayolipa. Ninavyoongea na wewe hivi sasa, sijaoga,
kama unataka nikuoneshe ushahidi nitakuonesha kama una shaka juu ya haya
yote nisemayo; sijaoga tangu mwaka 2001 hadi wakati huu."kwa sababu alimbiwa na Mungu asioge
Nadhani ulishawahi kusikia ama kushuhudia watu wa eneo Fulani ama jamii fulani wakimlazimisha kichaa kuoga kwa nguvu kwa kuwa amezidi kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa waumini wa dhehebu analolisimamia mchungaji Wale Olanguji wa Nigeria.
Mchungaji adai hajaoga tangu mwaka 2001 kwa sababu alimbiwa na Mungu asioge
Nadhani ulishawahi kusikia ama kushuhudia watu wa eneo Fulani ama jamii fulani wakimlazimisha kichaa kuoga kwa nguvu kwa kuwa amezidi kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa waumini wa dhehebu analolisimamia mchungaji Wale Olanguji wa Nigeria.
Mchungaji Wale wa kanisa la Divine Seed of God wa Ibadan, Oyo,
Nigeria ameliambia jarida la People City la Nigeria kuwa hajawahi kuoga
tangu mwaka 2001 wakati ambapo anadai alipokea amri ya Mungu ikimtaka
afanye hivyo na kwamba ajitenge na mkewe na kuacha kutumia baadhi ya
vinywaji.
Cha ajabu, licha ya kukaa miaka 13 bila kuoga mchungaji huyo hatoi
harufu na ni vigumu kumshitukia hadi akuoneshe mwenyewe vielelezo!
Hivi ndivyo mchungaji huyo alivyoliambia jarida hilo wakati
lilipomkumbusha kuwa mwaka 2001 alitoa maelezo kuwa Mungu amemwambia
asioge:
"Ndiyo, ni miaka 13 hadi sasa kwa ufupi. Mwaka 2000 mwanzoni Mungu
aliniambia niache kuoga, nijitenge na mke wangu na kwamba natakiwa
kuacha kutumia vinywaji vyote laini pamoja na wines. Na tangu wakati
huo…kwa kweli, nimekuwa nikifuata yote hayo.
0 comments:
Post a Comment