MAELFU YA WATU WAKWAMA MAPEMA LEO KWENYE STAND KUBWA JIJIN DAR ES SALAAM UBUNGO.
Mabasi yaendayo Dar es Salaam yakiwa yamezuiliwa katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu, Morogoro baada ya eneo la Ruvu mkoani Pwani kujaa maji. Picha na Juma Mtanda
Dar es Salaam. Uharibifu wa barabara uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, umeendelea kuwatesa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mbalimbali nchini hasa baada ya mabasi ya
mikoani kuzuiwa kufanya safari zake jana.
Amri ya kuzuia mabasi hayo ilitolewa jana ikiagiza mabasi yote yasiondoke katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo hadi itakapotangazwa vinginevyo, kutokana na uharibifu wa Barabara za Kilwa, Morogoro na Bagamoyo ambako madaraja yamevunjika.
Dereva wa Basi la Adventure liendalo Kigoma, Joseph Luciano alisema walitangaziwa na Sumatra na trafiki kuwa wasubiri mpaka hapo watakapojulishwa kuondoka.
“Hatuwezi kuondoka mpaka Serikali itakapotangaza ili kuepuka faini ambayo wenzetu, wale wanaopakia nje, wametozwa,” aliongeza huku ikielezwa kuwa baadhi ya mabasi yalitozwa faini kwa kukiuka amri hiyo.
Abiria anayesafiri kwenda Kibondo, Kigoma, Lydia Lutakinikwa alisema: “Nilikuja kuchukua mzigo wa duka langu tangu Ijumaa na nimekuwa nikilala gesti. Nimeishiwa hela hivyo nalazimika kuendelea kuwapo kwenye hili basi kwa kuwa sina tena pesa ya kwenda kulipia malazi.”
Kondakta wa Basi la Taqwa liendalo Nairobi, Yahaya Maulid alisema wameruhusu kubadilishwa tiketi za abiria wao, kama walivyoelekezwa na mamlaka husika ili kutoa nafasi kwao kujipanga upya.
Mkuu wa Usalama Barabarani Ubungo, Inspekta wa Polisi, Yusuf Kamutta alisema zaidi ya mabasi 400 yameathiriwa na uamuzi huo... “Tumezuia mawakala wasitoe tiketi mpya kwa sababu abiria wa leo (jana) ndiyo wanaotarajiwa kusafiri kesho, hivyo wanaweza kuuza tiketi za kuanzia keshokutwa.”
0 comments:
Post a Comment