Msanii Kizito adaiwa kukiri kuhusika katika Ugaidi dhidi ya Nchi yake
Msanii
wa muziki Kizito Mihigo kutoka nchini Rwanda amedaiwa kukiri kuhusika
katika matukio ya kigaidi yaliyokuwa na lengo la kuiangusha serikali ya
nchi hiyo, na hii ikiwa ni siku kadhaa tangu alipokamatwa na kuwekwa
kizuizina kwa mashtaka haya.
Kizito Mihingo
Mihigo
pamoja na wenzake wawili wanatuhumiwa kushirikiana na waasi wengine wa
kabila la Kihutu kutoka huko Afrika Kusini na Dr Kongo katika njama za
kupanga mashambulizi kwa ajili ya kuiangusha serikali.
Hata hivyo ripoti nyingine zinamtaja Mihigo kama mtu ambaye alikuwa karibu zaidi na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF), na kukamatwa kwake kumekuwa jambo ambalo linashtusha wengi.
Hata hivyo ripoti nyingine zinamtaja Mihigo kama mtu ambaye alikuwa karibu zaidi na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF), na kukamatwa kwake kumekuwa jambo ambalo linashtusha wengi.
0 comments:
Post a Comment