Msemaji wa P-Square azungumzia habari za kuwepo ugomvi mkubwa kati yao uliomhusisha kaka yao na mke wa Peter
Wiki hii mitandao ya Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na
ugomvi mkubwa kati ya mapacha wanaounda kundi la PSquare, Peter na Paul
Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.
Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao mkubwa ambaye ni meneja
wao, Jude Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda ameachana
na kundi hilo baada ya kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na
msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayofanyika
Dubai.
Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo.
“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.” Alitweet Jude Okoye.
Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo anaejulikana kama Bayo Adetu
amekanusha habari hizo wakati akiongea na Premium Times na kudai kuwa
hafahamu habari hizo zimetoka wapi.
“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know
where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to
their site. It’s baseless and untrue.” Amesema Bayo Adetu.