KWA MUJIBU WA JARIDA LA PEOPLE, HUYU NDIYE MWANAMKE MZURI ZAIDI DUNIANI MWAK
Lupita
ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12
years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii
ya jarida hilo.
Katika
orodha yake ya wanawake 50 warembo duniani,Lupita amewapiku waigizaji
maarufu akiwemo Kerry Washington, ambaye pia alishiriki katika filamu
hiyo na mwanamuziki Pink ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5
mtawalia.
Jarida la People limemtaja Lupita kuwa mwanamke mrembo
Stacy
Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.
Hatua
ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani na
kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke mrembo
duniani, ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga vichwa
vya habari nchini Marekani tangu kushinda
Mtandao
wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana kutajwa na
jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana kama yeye
watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.
"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.
0 comments:
Post a Comment