TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI
Home » » tisha xna

tisha xna

Chukua hiyo: Mtoto aliyejifungua akiwa na miaka 5 ndiye mzazi mwenye umri mdogo kuwahi kutokea, alimlea na kumsomesha mwanae

Wapo wanaoamini Mungu anaweza kufanya kila kitu. Wapo wanaoamini Sayansi ndiyo kila kitu na mahesabu hayadanganyi, wapo wanaoamini vyote kwa pamoja na wapo ambao hata kimojawapo hawakiamini! Naaamini wewe upo kati niliowataja, lakini kwa habari hii naamini utahamia ama utaendelea kuwa kama mimi niliye kwenye kundi la sentensi ya kwanza.
Wiki hii gazeti la Daily Mail la Marekani limeripoti habari ya watoto wanaoaminika kuwa wazazi wenye umri mdogo zaidi walio hai ambapo mtoto wa miaka 12 amejifungua na amezaa na mtoto wa miaka 13.
Lakini kabla haujashangaa, ningependa ufahamu kuwa katika historia ya binadamu mtoto wa miaka 5 aliwahi kujifungua na akamlea mwanae kama kawaida!
Ni hivi, Lina Medina ambaye anatajwa kuwa msichana aliyejifungua akiwa na umri mdogo zaidi, alizaliwa katika mkoa wa Ticrapo nchini Peru September 27, 1933 na alibahatika kujifungua mtoto wakati akiwa na umri wa miaka mitano, miezi saba na siku 17 tu.
Lina alipelekwa hospitalini na wazazi wake baada ya kugundua kuwa tumbo lake lilikuwa limeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikiriwa kuwa anaugonjwa lakini baada ya kufanyiwa vipimo, Dr. Gerardo Lozada aligundua ana ujauzito na hivyo yakamshinda akaamua ampeleke kuko Lima, Peru ili akaangaliwe na wataalam wengine kuthibisha kile alichokiona.
Lakini July, 16 mwaka 1936 magazeti yaliripoti kuwa mtoto huyo amepelekwa katika wodi ya taifa ya wazazi. Gazeti la San Antonio Light lenyewe liliripoti kuwa mtoto huyo pia angesafirishwa kwenda Marekani kutembelea chuo kikuu cha wataalam wa masuala ya afya, huku gazeti la La Cronica likitoa habari kuwa kampuni ya filamu ya Marekani Kusini ilimtuma muwakilishi akiwa na kitita cha $5,000 ili wampe mtoto huyo kwa lengo la kumshuti filamu lakini inaripotiwa kuwa walikataliwa.
Hata hivyo, La Cronica liliripoti kuwa Dr. Lozada mwenyewe alitengeneza makala fupi ya filamu ya kisayansi na aliionesha wakati akitoa ujumbe kuhusu masuala ya afya kwa umma.
May 14, 1939, Lina Medina alijifungua salama mtoto wa kiume mwenye kilo 2.7 lakini kutokana na viungo vyake vya uzazi kuwa vidogo, alilazimika kufanyiwa upasuaji na timu ya madaktari akiwemo Dr. Lozada, Dr. Busalleu na Dr. Colareta.
Mtoto huyo wa kiume alipewa jina la Geraldo ambalo ni jina la Daktari wake na aliishi na mama yake kwa muda miaka 10 akidhani ni dada yake, na mwisho wa siku akafahamu kuwa huyo ndiye mama yake mzazi.
Lilikuwa jambo la kushangaza sana! Lakini ilishangaza zaidi pale Dr. EdmudO Escomel aliandika katika journal ya La Presse Medicale kuwa Lina Medina alikuwa akipata mzunguko wa mwezi kama wanawake wakubwa tangu akiwa na umri wa miaka mitatu na akiwa na umri wa miaka 4 alikuwa na matiti makubwa kama binti mkubwa.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa walipomchunguza walikuta tayari alikuwa na organs ambazo zilikuwa tayari kwa kupata mtoto.
Suala la baba mzazi wa mtoto huyo lilizua utata mkubwa na Lina Medina alikuwa zaidi ya msiri na hakuwahi kumtaja kabisa baba wa mtoto wake hata alipoulizwa na madaktari kirafiki.
Ilikuwa hatari kwa baba mlezi wa Lina Menina ambaye alitupwa selo kwa muda mrefu akidhaniwa kuwa ndiye aliyempa ujauzito mtoto huyo, lakini aliachiwa baadae baada ya ushahidi kukosekana.
Msichana huyo alikuwa na akafanya kazi katika Clinic ya Dr. Lozad na kupewa elimu kuhusu masuala ya afya na alimsaidia kumsomesha mtoto wake hadi high school.
Baadae Lina Medina aliolewa na Raul Jurado na akapata mtoto wa pili mwaka 1972.
Hata hivyo, Medina hakutaka kabisa kufanya mahojiano na vyombo vya habari hata aliposhawishiwa sana na
Share this video :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | WILLE Template | GOOGLE
Copyright © 2013. Dj Wille Zedon - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger