HAWA NDIYO WASANII 8 WA BONGO MOVIES NA BONGO FLEVA WANAOPENDWA SANA NA JAMII..!!
Ukiachilia mbali wingi wa wasanii wanaofanya vizuri kwenye
tasnia mbali mbali apa bongo, sio wote wanaobahatika kukubalika na
kupokelewa vizuri na Jamii/mashabiki. Hawa ndio wasanii wenye mvuto
zaidi na wanaoongoza kwa kupendwa na mashabiki.
1.DIamond platinum
Anaweza akawa sio muimbaji mzuri kama Alikiba au barnaba, ila haina
ubishi huyu ndiye msanii wa kiume kwa upande wa bongo fleva anayeongoza
kwa kupendwa zaidi na mashabiki, jina lake linazidi kukua siku hadi siku
na kazi zake zinafanya vizur karibia east Africa nzima.
2. Wema sepetu
Sio muigizaji mzuri kumshinda Johari, wala hana filamu nyingi sokoni
kuliko Irene uwoya, ndio maana hata waandaji wa tunzo za filamu
hawajawahi kum nominate hata kwenye category ya msanii chipukizi bora,
hiyo haijafanya jina lake lishuke kwenye Tasnia hiyo, Bado haina ubishi
wema ana nyota Kali na anapendwa kuliko msanii yeyote. mwenyewe anajiita
ENDLESS FAME.
3. LADY JAYDEE
Kiuno chake kina mfupa, hana mauno makali kumzidi Snura mushi, sauti
yake nzuri na kipaji cha pekee alichobarikiwa kimemfanya apendwe zaidi
na mashabiki kibao. Unadhani ana pesa sana kuliko ruge? Hakustahili
kabisa kushindana naye , ila jeuri ya mashabiki aliyonao ilimfanya
ajione malkia , nadhan unakumbuka Team anaconda ilifanya nini pale
Nyumbani Lounge. Jide ana nyota Kali sana.
4. JB
Kipaji chake hakikumfikia marehemu kanumba(r.I.p),sio director mzuri
kama Jackson kibirigi, ubunifu alionao kwenye filamu zake umemfanya
apendwe zaidi na mashabiki kuliko msanii yeyote wa kiume kwa upande wa
filamu apa bongo.
5.Lulu Michael
Hajawahi kuigiza vizuri kama Diana kimaro(Danija,Kigodoro) ila ana nyota
nzuri sana, licha ya umri mdogo alionao , anapendwa na ana mashabiki
wengi zaidi.
6.Monalisa
Hana umbo kama masogange, kipaji cha kipekee alichonacho na umakini
alionao kwenye uigizaji umemfanya ajiongezee mashabiki wengi zaidi.
7. Ray kigosi
Sio muigizaji mzuri kumshinda Gabo, kampuni makini aliyonayo na aina ya
waigizaji anaowatumia imemfanya kazi zake zinunuliwe zaidi kuliko
kampuni yeyote apa bongo. Steps ilishawahi kusema kuhusu kazi za
waigizaji zinazonunuliwa kama njugu, ray alishika namba mbili
akitanguliwa na kanumba.
8.Johari
Hana swagger kama wema sepetu, kazi zake na umakini alionao kwenye
uigizaji , vimemfanya apendwe zaidi na mashabiki , ndo maana hadi Leo
kazi zake zipo juu.
cedit.swahili tz
0 comments:
Post a Comment