WACHINA WAKAMATWA NA MAKOMBE FEKI YA KOMBE LA DUNIA ZAIDI YA 1,000
NDOTO ya mashabiki wa timu ya Taifa ya England `Simba watatu` ni kunyanyua kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Lakini
suala hili limechukua sura mpya na shukurani za dhati
ziwaendee viongozi wa desturi wa China waliofanikisha kukamata mzigo
feki.
Nchi
ya China imekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya elfu moja (
1,000) katika ghala ya kampuni moja kubwa ya usafirishaji nchini humo.
Makombe
hayo feki 1, 020 ya kombe la dunia yamekamatwa katika mji wa Yiwu,
jimbo la Zhejiang, ambalo ni moja ya miji mikubwa ya usafirishaji wa
bidhaa duniani.
Makombe hayo feki kwa asilimia kubwa yanafanana na makombe halisi ya FIFA na yalikuwa tayari kusafirishwa kwenda nchini Libya
0 comments:
Post a Comment