Watu 682 wahukumiwa kifo nchini Misri, wengine 492 wavuliwa kitanzi, ndugu zao wazirai
Jaji wa mahakama ya Misri amewahukumu kifo watu 683
walitajwa kuwa wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood baada ya kukutwa
na hatia katika makosa ya kushambulia kituo cha polisi mjini Minya mwaka
jana ambapo polisi mmoja alikufa.
Kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood, Mohammed Badie ni miongoni
mwa watu hao waliohukumiwa kifo ambapo ilielezwa kuwa vurugu
walizoanzisha zilisababisha watu wengi kupoteza maisha.
Ripoti zinasema kuwa jamaa wa watuhumiwa waliokuwa wanasubiri nje ya mahakama walizirai baada ya kupokea taarifa za hukumu hiyo.
Katika hatua nyingine, Jaji wa mahakama hiyo pia amebatilisha hukumu
ya kifo iliyotolewa kwa watu 492 kati ya watu 529. Hukumu hiyo
ilipitishwa mwezi uliopita na watu hao wamehukumiwa kifungo cha maisha
jela.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu limekosoa
vikali mwenendo wa kesi hiyo na hukumu iliyotolewa ambapo imedaiwa kuwa
kesi hizo zilisikilizwa masaa machache huku mahakama ikiwazuia mawakili
kuwawakilisha washitakiwa.
0 comments:
Post a Comment