MASHABIKI WA CHELSEA NA LIVERPOOL WATWANGANA ANFIELD
VURUGU ilizotokea nje ya Uwanja wa Anfield kufuatia Liverpool kufungwa na Chelsea mabao 2-0 jana.
Picha
zinaonyesha kitimutimu cha maana nje ya Uwanja wa Anfield Road baada ya
mashabiki wa Liverpool kuwavaa mashabiki wa Chelsea waliokuwa wakiimba
jina la Nahodha wa Wekundu hao, Steven Gerrard baada ya mechi.
Shabiki mmoja alitupa konde kwa mwenzake, wakati wengine walitenganishwa na Polisi.
Makosa
ya Gerrard yalisababisha bao la kwanza la Chelsea lililofungwa na Demba
Ba na mashabiki wa The Blues wakawatia hasira Liverpool kwa kuimba jina
la mchezaji huyo.
Zomea zomea: Mashabiki wa Chelsea wakizomea kwa jeuri ya ushindi wa 2-0
Wawili tu: Mashabiki wakizipiga chanzo ni kuzomewa kwa Steven Gerrard
Polisi wakituliza ghasia
Sio salama: Baba akiongozana na kijana wake kutoka eneo la vurugu huku watu wakiendelea kuchapana nyuma yake
Ilikuwa si mchezo: Polisi walilazimika kuwaachanisha watu wengine waliopelekana hadi chini katika mapambano yao
Wakorofi: Polisi wakiwwka uzio baina ya mashabiki wa Liverpool na Chelsea
Waacheni tuwachape: Mashabiki wa Liverpool wakisema na Polisi waliokuwa wakituliza ghasia hizo
0 comments:
Post a Comment