Jackline Wolper Ampiku Agness Masogange Kwa Pedeshee Wa Kihindi, Ni Yule Aliyetoa Milioni 40 Kwa Ajili Ya Kumchumbia Masogange
Msanii Wolper akiwa na Prence Kass maarufu kama Muhindi wa Masogange |
Na Sakina Shabani
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Xdeejayz imenasa picha za msanii nyota wa filamu za Kibongo Jackline Wolper akiwa na mfanyabishara mmoja wa kihindi mwenye pesa ndefu aliyefahamika kwa jina la Prence Kass maarufu kama Muhindi wa Masogange.
Picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa kwenye moja ya viunga vya Club ya usiku iliyopo Oysterbay/ Masaki ambapo hata hivyo uhalisia wa picha hizo unamuonesha Wolper akiwa bwii kiasi cha kuubetua mdomo wake ambapo sio kawaida kwa mtu mwenye ufahamu na staa kama yeye kupiga picha zenye pozi baya kama hizi.
Prence Kass ambae aliwahi kumchumbia Agness Masogange hadi kwa mjombaake na msichana huyo anawafunika mastaa wote bongo kwa makalip yake tata na kila kitu kilikuwa kinaenda swa kuhusu suala la kumuoa kwani Prence alishamtengea zaidi ya milioni 40 ili kumuachisha na mambo ya sanaa ili amfungulie maduka.
CREDIT (DJ WILLE ZEDON BLOG TANZANIA)
0 comments:
Post a Comment