Yule tajiri Mmarekani aliesema hataki watu Weusi..hatiwaye afungiwa Maisha
NBA
imesema kutokana na uchunguzi kukamilika kuhusu mmiliki wa timu ya Los
Angeles Clippers Donald Sterling dhidi ya maneno ya kibaguzi kwa watu
weusi, imempa kifungo cha maisha mmiliki huyo mwenye umri wa miaka 80.
Wanasema baada ya kufanya uchunguzi Donald amekubali kwamba sauti
iliyosikika ikitoa maneno mazito ya kibaguzi dhidi ya watu weusi ni ya
kwake ambapo alikua akiongea na Mwanamke anaedaiwa kuwa mpenzi wake.
Donald ambae aliwahi kukiri siku kadhaa zilizopita kwamba hatoiuza
hii timu, kwenye adhabu ya maisha aliyopewa ni kwamba hatoruhusiwa
kuhudhuria mazoezi ya timu yake wala kwenda kwenye game zote maishani
mwake na vilevile hatoruhusiwa kufanya maamuzi yoyote kwenye timu.
Kingine kilichoongezeka ni faini ya dola za Kimarekani milioni 2.5 ambazo kibongobongo inagonga kwenye 4107500000
ambapo inasemekama hii sauti ya Sterling akitoa maneno ya kibaguzi
ilirekodiwa September 2013 na kwamba alishtukia kwamba karekodiwa.
Yote
haya yametokana na kuvuja kwa sauti ya mazungumzo kati yake na
girlfriend ambapo Donald Sterling aliongea maneno makali ya kibaguzi kwa
kusema kwamba hataki girlfriend wake ajihusishe na watu weusi kwa
kupiga picha au kwenda nao kwenye mechi.
Imeshangaza
zaidi kwa sababu timu yake ina wachezaji mashuhuri weusi kama Chris
Paul na Blake Griffin aliyewahi kucheza ligi ya chuo pamoja na Mtanzania
Hasheem Thabeet lakini wakiwa wanatoka kwenye vyuo tofauti.
Kamishna wa NBA amesema atatumia nguvu ya uongozi wake kuhakikisha L.A Clippers haimilikiwi tena na Donald Sterling.
0 comments:
Post a Comment