Fid Q kuoa hivi karibuni lakini.. sio Mama Feisal, aeleza jinsi mama yake Salama Jabir alivyohisi ana uhusiano na bintiye!
Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q, amesema yupo mbioni kuukacha ukapela. Hata hivyo anasema kuna kikwazo kikuu kimoja katika kufanikisha hilo.
“Kiukweli kabisa naomba niwe muwazi, natarajia kuoa hivi karibuni lakini nakumbana na vikwazo vingi sana coz nina mtoto,” rapper huyo mshindi wa tuzo za KTMA 2014 ameiambia Global TV. “Unajua unapokuwa na mwanamke halafu una mtoto wa nje inakuwa ni ngumu kumfundisha mtoto aweze kuelewa kuwa siyo mama yake. Kwa hiyo hicho ndicho kitu nakutana nacho lakini inshaallah Mwenyezi Mungu nimemtanguliza mbele nimempata ambaye ananifaa na muelewa,” aliongeza.
Fid na Salama
Katika hatua nyingine akijibu swali la kama alishawahi kuwa na uhusiano na Salama Jabir, Fid alisema:
Hilo swala siyo kweli, hizo tetesi sishangai kusikia kwako hata kwa Watanzania wengi wameshawahi kuhoji na zaidi mama yake, pia alishawahi kuhisi hivyo nadhani ni urafiki wetu wa karibu ambao ulikuwa mkubwa zaidi na ilikuwa ni ngumu kuamini kama tunaweza kuwa marafiki wa kawaida, ieleweke kuwa Salama ni mshikaji wangu tu na hakuna mambo mengine yoyote ya faragha.”

0 comments:
Post a Comment