Master Jay "Uchawi Bongo Flava Upo Nimewahi Kuona Msanii Anatoa na Panzi Kooni"
Producer mkongwe wa muziki na mmliki wa MJ Records, Master J, amesema
uchawi upo kwenye muziki na ameshawahi kushuhudia msanii wa bendi
akitolewa panzi kooni iliyoingia kimazingara ili ashindwe kuimba.
Akiongea na kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio jana, Master J
amesema wapo baadhi ya wanamuziki wanaojihusisha na masuala ya
ushirikina.
“Hivi ni vitu vya kawaida, huu ni utamaduni wetu,mimi sishangai wala
sioni kitu chochote cha ajabu. Mimi nilianza kwa kurekodi muziki wa rap
tu, lakini baadaye nikaanza kurekodi band, Taarab na mchiriku ndio maana
nishasemaga nimeshawahi kuona kwenye band mtu anatoa panzi kabisa
kutoka kooni, akafanyiwa maujanja ndo akaweza kuimba. Kusikia wasanii wa
Bongo Flava wanajihusisha sio kitu cha ajabu kwani wao si ni Watanzania
na Tanzania taka usitake utamaduni wetu ni uchawi, uchawi upo,kwahiyo
mimi sishangai,” alisema.
0 comments:
Post a Comment