Kuibuliwa kwa Picha hiyo kumekuja Siku chache kufuatia mgombea huyo kutangaza nia huku akianika kipaumbele chake endapo atapata ridhaa ya wapiga kura ikulu.
Nikama kumekucha!Tayari mbinu za kuchafuana na kupakana matope miongoni mwa wanasiasa waliojitokeza kugombea Urais kupitia chama kimoja cha Siasa zimeanza kujitokeza baada ya hivi karibuni kuibuliwa kwa picha ya mgombea mmoja wa chama hicho aliyetangaza nia akiwa na hawara ndani ya chumba cha Hoteli.
Kwamujibu wa Chanzo cha HAabari kilichotinga katika Ofisi za Global Publishers Bamaga-Mwenge,inadaiwa kuwa muheshimiwa huyo(jina tunalo) na mwanamke huyo ambaye si mke wake,walipiga picha hiyo muda mrefu lakini kutokana na duru la kisiasa za uchaguzi mkuu mwaka huu,Picha hiyo inaonekana kuwa 'keki' kwa wapinzani wake.
"Unajua hii picha ni ya muda mrefu.Mheshimiwa alipiga akiwa na uhusiano na huyu mrembo.sasa mhesahimiwa alipotangaza nia tu,wabaya wake wakaona hapa ndiyo penyewe,wakaiibua ili itumike kwenye kampeni yake ya urais kama chama chake kitampitisha yeye kugombea,''kilisema chanzo
0 comments:
Post a Comment