Video Director anaefanya vizuri hapa Bongo kwa kutengeneza Hit kama ya Pacha wangu ya Rich Mavoko ajulikanae kama Adam Juma amesema anatamani siku moja atengeneze msanii mwenye mafaniko kama alionayo Diamond Platnumz.
Akiongea katika 255 ya XXL amesema:
"Natamani kupata ngoma kali, natamani mtu aimbe nyimbo nzuri haijalishi ni msanii gani, sina wigo wa kusema nifanye kazi na msanii flani mkubwa sina msanii mkubwa sina msanii mdogo, naamini saizi nachotaka kufanya kuna mtu ameshatuonesha moyo Diamond alipofikia, the whole entire of Afrika wanamtaka, nataka kumtengeneza mwingine, nataka kumtengeneza mwingine kutoka chini kabisa asimame, kwasababu bado nina ndoto, bado nina vitu kichwani kwahiyo msanii yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi anaweza kufanya kazi na mimi."
0 comments:
Post a Comment